Kiongozi wa chama cha Wiper nchini Kenya, Kalonzo Musyoka amesema kuwa Raila Odinga ataapishwa iwapo Rais Uhuru Kenyatta hatakubali kufanya mazungumzo na upinzani.

Amesema kuwa mipango ya kuapishwa iko katika maandalizi na suala hilo haliwezi kuzuiliwa na mtu yeyote hivyo Wakenya wajiandae kwaajili ya sherehe hizo.

Kalonzo amesema haikubaliki kwa Rais kulinganisha juhudi zao za kufanya mazungumzo kulinganishwa kuwa ni sawa na kufanyika uchaguzi wa urais 2022 na kwamba hawatarudi nyuma.

“Hivi Rais hana moyo? Moyo wangu unavuja damu. Mimi na kaka yangu Raila tutaendelea na sherehe za kuapishwa kama rais na makamu wake wa wananchi iwapo hatozingatia wito wetu wa kuwepo mazungumzo ili kuondoa dhulma ya uchaguzi katika nchi hii. hatuwezi kusimamisha kuapishwa kwetu,” amesema Musyoka

Hata hivyo, Mahakama ya Juu nchini Kenya ilibatilisha ushindi wa Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 8 kufuatia Raila kupinga matokeo hayo na kutaka marudio ya uchaguzi yafanyike Oktoba 26, ambapo Rais Kenyatta alishinda baada ya viongozi wa NASA kususia uchaguzi huo.

Dk Shika aiaga bongo
Picha: Zitto aanika madeni na rasilimali zake