Muungano vyama vya upinzani nchini Kenya, (NASA) ambao ulishindwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, umeapa kuendelea kufanya maandamano yenye nia ya kubatilisha kile ambacho wanasema kuwa matokeo feki ya uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa na Seneta James Orengo ambapo amesema kuwa muungano wa vyama vya upinzani NASA unaoongozwa na Raila Odinga hautapinga matokeo ya uchaguzi kupitia mahakama kwani Kenyatta tayari ametoa vitisho kwa majaji.
Aidha, kufikia sasa watu 11 wameuwawa katika ghasia za baada ya uchaguzi mkuu, ambazo zilianza mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kushinda na kutangazwa mshindi kwa muhula wa pili usiku wa kuamkia Jumamosi.
Kwa upande wake kiongozi wa upinzani, Raila Odinga amedai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki kwani matokeo hayo yalichakachuliwa hivyo hayatambui matokeo hayo.
Hata hivyo, Tume ya kutetea haki za binadamu nchini Kenya, imetoa orodha ya waathirika wa ghasia hizo huku ikisema kuwa ni watu 24 ndio ambao wameuwawa katika vurugu hizo zinazohusishwa na uchaguzi huo, huku ikiongeza kuwa polisi wanatumia nguvu kupita kiasi