Manchester United imeshuhudia ofa yake ikikataliwa na Inter Milan kwa ajili ya kipa, Andre Onana, na kwa sasa Uongozi wa klabu hiyo unajipanga kuwasilisha ofa mpya.

United inapambana kupata saini ya Onana ambaye kwa sasa ni lulu Barani Ulaya kutokana na ubora wake.

Ofa ya Pauni 34.4m ziliwekwa mezani na Man United kwa Inter Milan pamoja na Bonasi ambapo jumla inafika pauni 38.5m, lakini ikakataliwa.

Inter Milan wanataka Pauni 44m ili kumuachia Mlinda Lango huyo kutoka nchini Cameroon.

Ikumbukwe kuwa, United wanapambana kupata saini ya Onana ili kuziba nafasi ya David de Gea ambaye kwa sasa yupo huru japo mazungumzo yanaendelea, huku muafaka wake haujajulikana.

De Gea ambaye ni Mlinda Lango chaguo la kwanza la United, mkataba wake ulimalizika Juni 30, 2023, kwa sasa yupo huru kuondoka ingawa haijawekwa wazi.

United ni kama inataka kumuachia De Gea kutokana na kuwa ndiye mchezaji anayechukua mshahara mkubwa wa wiki kiasi cha pauni 375,000.

Kuondoka kwa De Gea itakuwa afadhali kwa klabu hiyo kupunguza matumizi ya fedha.

Onana amefanikiwa kufanya kazi na Kocha Erik ten Hag akiwa Ajax, msimu uliopita wa 2022-23 alitisha akiwa na Inter Milan mpaka kufika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mbali na Onana, Man United inapambana kuhakikisha inapata kipa ambaye atakuwa msaada kwa timu.

Kocha Nkoma atoa ushauri wa bure WPL
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 7, 2023