Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris St-Germain (PSG) umepanga kumsajili Mshambuliaji kutoka nchini Nigeria na Klabu ya Bingwa Italia SSC Napoli, Victor Osimhen katika dirisha hili la usajili linaloendelea Barani Ulaya, endapo Kylian Mbappe ataondoka jijini Paris.

Taarifa zinadai PSG inataka kumuuza Mbappe katika dirisha hili na ikishindikana itapambana kurefusha mkataba wake hadi 2025.

Taarifa kutoka Italia zinaeleza kwamba PSG imeshatuma ofa ya kwanza ya Euro 100 milioni kwenda SSC Napoli, lakini ilikataliwa na kuambiwa kwamba ikihitaji huduma ya Osimhen itatakiwa kutoa zaidi ya Euro 180 milioni na hiyo ndani ya msimu huu tu kwani timu yake imepanga msimu ujao kupandisha dau zaidi kutokana na imani kwamba nyota huyo ataendeleza ubora ambao amekuwa nao kikosini.

PSG iliachana na mpango wa kutaka kumsajili nyota huyu wa kimataifa wa Nigeria mwenye umri wa miaka 24, kwa sababu haikuwa na uhitaji mkubwa, lakini kitendo cha Mbappe kuhusishwa kuondoka kinaonekana kuifanya idhamirie kweli kumsainisha mkataba mchezaji huyu ili akawe mbadala wake huko Ufaransa.

Vilevile timu hiyo ambayo ni bingwa mtetezi wa Ligi Kuu Ufaransa (Serie A) inadaiwa kwamba itatumia mkwanja itakaoupata kwenye mauzo ya Mbappe anayehusishwa na Real Madrid ili kukamilisha usajili wa Osimhen ambaye msimu uliopita alifunga mabao 31 katika mechi 39 alizocheza, huku akitikisa katika Ligi Kuu Italia.

Mkataba wa sasa wa Osimhen unatarajiwa kumalizika ifikapo 2025, lakini lolote linaweza kutokea msimu huu.

Waarabu wa Saudia wahamia kwa Pogba
Ulinzi ni wakati wote sehemu zote nchini: Misime