Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, Samweli Komba amewazuia kwenda likizo wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu ili watumie likizo hiyo vyema katika kujifunza.
Amesema kuwa ameamua kufikia maamuzi hayo ya kuwazuia watoto kutorudi nyumbani ili kuwafanikisha watoto ambao wapo Shuleni na hawajaweza kufanikiwa kuzijua K.K.K. kujifunza kwa umakini na ukaribu na walimu.
Ofisa elimu huyo wa shule za msingi Mbinga, amesema kuwa hadi sasa wazazi wao wameshapewa taarifa pamoja na walimu wao ambao watakuwa wanawafundisha wanafunzi hao kipindi chote cha likizo.
“Hakuna muda mwingine ambao utamfanya mwanafunzi asiyejua K.K.K kujifunza kikamilifu zaidi ya kipindi hiki cha likizo,”amesema Komba
Aidha amongeza kuwa kuwepo kwa kwa baadhi ya wanafunzi ambao wenye afya timamu halafu hawajui KKK, ni jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho, na ameahidi kuzitembelea shule zote za msingi wilayani Mbinga kuona kama agizo limefanyiwa kazi.