Ofisi ya Makamu wa Rais, imewasilisha Taarifa kuhusu muundo na majukumu yake kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria katika Ukumbi wa Ofisi za Bunge jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amewasilisha taarifa hiyo ambayo pia imejadiliwa na Kamati hiyo ya Bunge kwa upande wa Muungano na kusema Serikali itaendelea kutoa elimu kuhusu Mfuko wa kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa upande wa Zanzibar.

Amesema, ipo haja ya kutoa elimu hiyo kwa viongozi wa mabaraza ya wilaya ili yaliyopo Zanzibar.
Akiendelea kuzungumza wakati wa kikao hicho, na kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itahakikisha wananchi wa pande zote mbili za Muungano wanafaidika na rasilimali zilizopo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Maji na Mazingira, Florent Kyombo ametaka ushauri uliotolewa na wabunge uzingatie huku baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakishauri iongezewe nguvu katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Wabunge hao pia wameshauri Ofisi ya Makamu wa Rais iendelee kufanya kazi kwa karibu na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), na kufuatilia kwa karibu wa miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali ya nchi ikiwemo Dodoma kwani baadhi ya miti inakufa.

Jisajili na ushinde Meridianbet mgao wa TZS 3,000,000 kwa 5,000
Polisi yawataka Waendesha Baiskeli kutii sheria usalama barabarani