Aliyekuwa Meneja wa Man Utd Ole Gunnar Solskjaer huenda akapewa majukumu mapya tofauti na Benchi la Ufundi la klabu hiyo endapo mwekezaji Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani atatua Old Trafford.

Mwekezaji huyo kutoka Qatar na bilionea kutoka Uingereza, Sir Jim Ratcliffe wanasubiriwa kuona ni nani atashinda katika kinyang’nyiro hicho.

Baada ya familia ya Glazer kuamua ni nani wanataka kumuuzia, mchakato wa kuidhinisha uliodumu kwa muda wa wiki nane kabla ya mkataba kusainiwa.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mirror, Sheikh Jassim yuko tayari kuwajumuisha wakongwe wa Man United katika uendeshaji wa klabu hiyo endapo atafanikiwa na mpango wake wa kuinunua.

Nyota wa zamani wa Man United, Solskjaer ambaye aliinoa anaripotiwa kuwa miongoni mwa magwiji wa klabu wanaoandaliwa kupewa shavu siku za usoni.

Solksjaer alifunga mabao 126 katika michezo 366 akiwa na Mashetani Wekundu, alishinda mataji sita ya Ligi Kuu ya England na akafunga bao la ushindi wa Ligi ya Mabingwa mwaka 1999.

Solskjaer aliinoa Man United kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kutimuliwa mwaka 2021 kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Kocha huyo raia wa Norway, aliweka wazi uwezekano wa kurudi Old Trafford endapo atavutiwa na majukumu hayo mapya.

Miquissone awavuruga mabosi Simba SC
Sanchez ampigia magoti Mikel Arteta