Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka ametuma salamu za rambirambi kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na kwa Mkuu mkoa wa Mwanza, John Mongela na waathirika wa ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV Nyerere kilichotokea katika kisiwa cha Ukerewe ziwa victoria mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ole Sendeka amewataka Watanzania kuungana katika kipindi hiki kigumu pamoja na kuliombea Taifa na kuwafariji waathirika badala ya kuendelea kufanya mambo ambayo yanaendelea kuleta sintofahamu kwa taifa.
“Tuwe wazalendo na kuenzi misingi yote ya taifa hili, Tunapaswa kuendeleza amani na uzalendo pamoja na misingi iliyowekwa na nchi yetu na hivyo basi watu wasitumie msiba huu kujitafutia umaarufu au mtaji wa kisiasa’’amesema Ole Sendeka.
Aidha, katika hatua nyingine Ole Sendeka amesema kuwa uongozi wa mkoa wa Njombe unaungana na mikoa mingine nchini kutoa rambirambi hiyo.
-
Rais awashika mkono wafiwa, manusura MV Nyerere, walamba mamilioni
-
Mtoto aliyepotea apatikana polisi
-
TCU yafuta vyuo lukuki
Hata hivyo, licha ya baadhi ya miili ambayo imeopolewa katika ajali hiyo na kufanyiwa maziko mnamo Sept 23 lakini bado serikali inaendelea na zoezi la kuitafuta miili ya waathirika wa ajali hiyo pamoja na kukinasua kivuko kilichopinduka.