Kwa kipindi cha miaka mingi iliyopita, nchi za Korea Kusini na Korea Kaskazini zimekuwa katika vita licha ya kuwa majirani na kutokana na historia ya vita vyao kuwa ya muda mrefu imechangia mpaka kizazi cha sasa cha mataifa hayo kimeendelea kutokuwa na mawaelewano mazuri baina yao.

Lakini licha ya mahusiano ya mataifa hayo kutokuwa mazuri, michezo ya ‘Olimpiki’ (Olympics 2016) ambayo inaendelea nchini Brazil inaonyesha wazi kuwa inaweza kuibua mahusiano mapya ya mataifa hayo mawili ambayo hayapatani.

Wanamichezo kutoka mataifa hayo mawili, Lee Eun-ju kutoka Korea Kusini na Hong Un-jong kutoka Korea Kaskazini wameonekana wakipiga picha ya pamoja “selfie” na wote wakiwa na nyuso za furaha jambo ambalo linatajwa kuwa linaweza kuibua mahusiano mapya baina ya mataifa hayo.

Mtaalam wa siasa kutoka Marekani, Ian Bremmer amelizungumzia jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kusema kuwa michezo ni njia ambayo inaweza kuunganisha kila mtu na hilo ndiyo dhumuni la kuwepo michezo kama ya olimpiki.

“Hii ndiyo sababu ya kufanyika Olimpiki, michezo inawaleta watu wote karibu,” alisema Bremmer.

Arsene Wenger Amnyatia Wilfried Bony
Lissu adai kushtukia njama za kuwavua ubunge yeye na Mbowe