Mlinda mlango wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani na klabu ya  Bayern, Munich Oliver Kahn ameteuliwa kuchukua nafasi ya mwenyekiti mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge kuanzia Januari 2022.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mabingwa hao wa kihistoria  nchini  humo wamesema   kwamba  Kahn  mwenye   miaka 50 , ambaye alikua nahodha  wa  zamani  wa  Bayern  na  mchezaji  wa  kimataifa  wa Ujerumani, amesaini mkataba  wa  miaka  mitano  na  klabu  hiyo utakaoanza  Januari 1, 2020, baada  ya  kuthibitishwa katika mkutano  wa  bodi  ya  utendaji mwishoni mwa juma lililopita.

Kahn ambaye  hivi  sasa  ni mfanyabiashara  na mtaalamu  wa masuala ya michezo katika runinga, amekuwa  akitajwa kwa  mara kadhaa  kuchukua  nafasi ya  Rummenigge  mwenye umri  wa  miaka 63, ambaye atajiuzulu wakati  mkataba  wake utakapofika kikomo Disemba 31, 2021.

“Ni heshima  kubwa  kwangu kwamba nitaaminiwa  kushika wadhifa katika  ofisi kama  mwanachama  wa  bodi  ya  bayern Munich na baadaye  katika  ofisi  ya  mtendaji  mkuu CEO na  mwenyekiti wa bodi  ya  utendaji ya Bayern Munich,” alisema Oliver Kahn.

Alikiba ''siishi kistaa kama watu wanavyosema''
Mrithi wa Lissu aapishwa Bungeni kwa kishindo, auliza swali la kwanza, Ndugai atoa neno