Wachezaji kutoka nchini England Lucy Bronze na Fran Kirby wameungana na mshindi mara tano wa tuzo mchezaji bora wa kike wa FIFA Marta, kwenye orodha ya wachezaji 15, wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kike ya Ballon d’Or kwa mwaka 2018.
Lucy Bronze amekua muhimili mkubwa katika klabu yake ya Olympic Lyon, na alifanikiwa kuisaidia kutwaa ubingwa wa 12 mfululizo wa ligi ya wanawake ya nchini Ufaransa, sambamba na ubingwa watatu mfululizo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Kwa mafanikio hayo klabu ya Olympic Lyon imefanikiwa kuwa na wachezaji saba kwenye orodha ya wachezaji 15, wanaowania Ballon d’Or kwa wanawake, ambayo itatolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Kwa upande wa Fran Kirby ambaye alishinda tuzo ya waandishi wa habari za michezo na tuzo ya wachezaji wa kulipwa nchini England mwishoni mwa msimu uliopita, amekua na msimu mzuri akiwa na klabu yake ya Chelsea.
Mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa wanawake atatangazwa Disemba 03, kwenye hafla itakayofanyika mjini Paris.
Orodha ywa wachezaji wanawake wanaowania tuzo ya Ballon d’Or
- Lucy Bronze (Lyon, England)
- Pernille Harder (Wolfsburg, Denmark)
- Ada Hegerberg (Lyon, Norway)
- Amandine Henry (Lyon, France)
- Lindsey Horan (Portland Thorns, United States)
- Fran Kirby (Chelsea, England)
- Sam Kerr (Chicago Red Stars, Australia)
- Saki Kumagai (Lyon, Japan)
- Amel Majri (Lyon, France)
- Dzsenifer Marozsan (Lyon, Germany)
- Marta (Orlando Pride, Brazil)
- Lieke Martens (Barcelona, Netherlands)
- Megan Rapinoe (Seattle Reign, United States)
- Wendie Renard (Lyon, France)
- Christine Sinclair (Portland Thorns, Canada)