Msanii  mkongwe wa nyimbo za kizazi kipya mwenye mchango mkubwa katika sanaa ya muzikiTanzania Rehema Chalamila maarufu kama Ray C katika kuingia mwaka mpya ametoa kali ya mwaka baada ya kumuomba Rais Magufuli asaidie kupatikana sheria itayosimamia wanawake na wanaume kutokuwa na mahusiano hadi ndoa.

Ambapo Ray C amesema kwa kufanya hivyo itasaidia wanawake na mabinti wa Tanzania kuolewa kwa haraka pia itasaidia wanaume kuoa.

Aidha amesema kuwa ameamua kuomba jambo hilo kwa kuwa amekuwa akishuhudia wanawawake wengi wakichezezewa na kuachwa pasipo kuolewa, hivyo sheria hiyo itarekebisha hilo kwa asilimia nyingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C aliandika hivi,

“Mzee mimi na shida moja, hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji sana! Ombi langu la mwaka huu kwako ni hili. Naomba upitishe sheria hakuna mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume mpaka wafunge ndoa! Na yeyote atakaekutwa na mwanamke iwe hotelini! Guest house bila cheti cha ndoa wapelekwe wote Segerea. Nadhani itasaidia sana wanawake wengi kuolewa badala ya kuwa manungaembe” amesema Ray C.

Kuoa au kuolewa ni jambo la kheri, na Ray C yupo sahihi kuwaza hivyo, kwa maoni yangu kama muhariri wanawake na wanaume watambue nafasi zao, ndoa nyingi zinafungwa siku hizi na hazidumu, tatizo linaanzia hapo.

Kikubwa ni kuwa na maadili tu, wanaume siku hizi kwenye mahusiano wanatembea na wadada wazuri warembo na watanashati lakini mwisho wa siku wanaishia kuoa mwanamke ambaye wa kawaida sana ‘Wife material”. Ni jambo ambalo wanawake wajiulize kwa kina sana.

Toa maoni yako kwa asilimia ngapi unamuunga mkono Ray c, je shida ipo wapi, na nini kifanyike?.

 

 

Trump atishia kuikatia msaada Palestina
Kiongozi wa Boko Haram aibuka tena