Subira na maombi ya mashabiki wa Ommy Dimpoz vimejibiwa na mwimbaji huyo amerejea rasmi baada ya takribani mwaka mmoja wa kupatiwa matibabu akiwa amelazwa hospitalini.
Mwimbaji huyo ambaye alifanyiwa upasuaji mkubwa mara kadhaa kutokana na kusumbuliwa na tatizo la koo, ameandika kwa mara ya kwanza ujumbe kwenye Instagram wenye maelezo kuhusu kuimarika kwa afya yake na shukurani.
Ommy ambaye ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Ni Wewe’ ambayo inazungumzia maisha yake tangu na jinsi Mungu alivyomponya.
“Mitihani, maumivu, huzuni na maombi ndio vitu vilivyotawala maisha yangu kwa miezi 12 iliyopita. 3 life threatening surgeries (upasuaji mara tatu unaohatarisha maisha), ila leo bado ni nimesimama Alhamdulilah,” ameandika Omy Dimpoz.
“Namshukuru Allah na wote tuliokuwa pamoja katika mapito yangu, sasa nimepata nafuu na nimeanza kurejea kazini taratibu. #Niwewe wimbo wa kuwapa faraja wote wanaopitia magumu. Video is Out, pita kwenye YouTube channel yangu na tuimbe kw apamoja utukufu wa Mungu. Produced by @yogobeats video Directed by @kevinboscojr @rockstarafrica,” aliongeza.
Kati ya watu waliojibu ujumbe wa Ommy kwenye Instagram, ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo pamoja na mkali wa RnB, Juma Jux.
“Kazi kazi baba Mungu ni mwema,” aliandika Jux. Jokate naye aliandika, “Mungu ni mwema pole sana Ommy @ommydimpoz.”
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kupitia Instagram alieleza kuwa alizungumza na Ommy Dimpoz kwa njia simu na kueleza kuwa amefurahi kuona kuwa hivi punde watarejea tena mazoezini pamoja.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ali Kiba ambaye ni mkurugenzi wa Rockstar Africa ambayo Ommy Dimpoz ni mwanafamilia, madaktari walisema chanzo cha tatizo lake la koo ni sumu.
Alitibiwa Afrika Kusini pamoja na Ujerumani, na sasa amerejea kwenye muziki baada ya afya yake kuimar