Uongozi wa klabu ya Mtibwa Sugar umesitisha mkataba wa Kocha kutoka nchini Cameroon Joseph Omog, baada ya kupata ushindi wao wa kwanza jana Jumapili (Desemba 12).
Mtibwa Sugar waliifunga Biashara United Mara katika Uwanja wao wa nyumbani Manungu Complex, baada ya kuambulia matokeo yasiyoridhisha kwenye mchezo saba tangu kuanza kwa msimu huu 2021-22.
Taarifa kutoka Mtibwa Sugar zinadai kuwa Kocha huyo amesitishiwa mkataba wake huku Salum Mayanga akionekana kwenye viunga vya Manungu, Turiani.
Hata hivyo haijaelezwa kwa kina kuonekana kwa Mayanga ambaye kwa sasa ni Kocha wa Tanzania Prisons, ni sehemu ya kutaka kumrejesha klabuni hapo kama Kocha mkuu.
Hii ni mara ya tatu kwa Kocha Omog kusitishiwa mkataba akiwa nchini Tanzania, aliwahi kufanyiwa hivyo akiwa Azam FC na Simba SC.