Kocha wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Wekundu wa Msimbazi Simba Joseph Marious Omog, ametangaza msimamo wake kuhusu mustakabali wa kiungo Mohamed Ibrahim “Mo”, ambaye anahusishwa na taarifa za kutakiwa kwa udi na uvumbwa na Young Africans.

Omog ameamua kufunguka, baada ya kusikia na kuona taarifa zinzomuhusu mchezaji huyo kupitia vyombo vya habari, huku ikielezwa kutomtumia mara kwa mara imekua chanzo Young Africans kujaribu kumfukuzia katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili.

Kocha huyo kutoka nchini Cameroon amesema, Mo ni mmoja kati ya wachezaji anaowahitaji zaidi katika kikosi chake, hivyo hayupo tayari kumuona akiondoka klabuni hapo.

Ameongeza kuwa, hata kama hatumiki mara nyingi, sio sababu ya kumruhusu kuondoka kwenye kikosi chake. Hivyo, ikiwa Young Africans wataendelea kusisitiza kuwa wanamuhitaji, basi kuna uwezekano mchezaji huyo akaongezewa dau katika mkataba wake mpya, kwa kuwa mkataba wa sasa unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Mo alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea kwa wakata miwa wa mkoani Morogoro Mtibwa Sugar, na amekua mchezaji mwenye bahati pindi anapopata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza ama kuingia kama mchezaji wa akiba.

Mwenyekiti Taifa BAVICHA aimwaga Chadema
Profesa Kitila azungumzia ‘tetesi’ za kugombea jimbo la Nyalandu