Klabu ya Manchester United imejipanga kumkosa Mlind Lango André Onana wakati wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) zitakazochezwa mwezi Januari 2024, ingawa golikipa huyo bado hajafanya uamuzi kama ataicheza Cameroon.
Kocha wa United, Erik ten Hag, anapanga kutomkosa Onana kwa muda wote wa michuano hiyo, itakayoanza Januari 13 hadi Februari 11, mwakani huko Ivory Coast.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kukosa mechi nne za Ligi Kuu England kama Cameroon itatinga fainali itakayochezwa Februari 11, mwakani.
Ten Hag hajafahamishwa rasmi, lakini Mholanzi huyo, kulingana na chanzo, anaelewa hali hiyo na atamruhusu Onana kufanya uamuzi wake kuhusu kushiriki au kutoshiriki.
United waliambiwa wakati wa mazungumzo ya kumsajili Onana kutoka Inter katika majira ya joto alikuwa amestaafu soka la kimataifa baada ya kuondoka mapema kwenye Kombe la Dunia kule Qatar.
Tangu wakati huo aliitwa kikosini kusaidia Cameroon kufuzu kwa AFCON na amechaguliwa kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Libya na Mauritius wakati wa mapumziko ya Novemba hii.
Chanzo kimoja kimeiambia ESPN Onana atafanya uamuzi wa mwisho kuhusu kusafiri na kikosi kuelekea Ivory Coast karibu na wakati na baada ya mazungumzo na Shirikisho la Soka la Cameroon.
United wanaamini wako tayari kwa uwezekano wa kuondoka kwa Onana baada ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uturuki, Altay Bayindir kutoka Fenerbahce majira ya joto.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 bado hajacheza mechi yake ya kwanza pale United lakini vyanzo vimeiambia ESPN tayari amewavutia katika mazoezi.
Kumpoteza chaguo la kwanza la Onana bado kunaweza kumfadhaisha Ten Hag, ambaye tayari anakabiliana na orodha ya majeruhi inayoongezeka.
Christian Eriksen na Rasmus Højlund ndio wachezaji wa hivi karibuni ambao wamepata matatizo na kujiunga na Lisandro Martínez, Casemiro, Luke Shaw, Tyrell Malacia na Jonny Evans wakiwa nje ya uwanja.