Ni vipi unaweza kuitambua thamani yako?

Kabla hujajibu hili swali, inakupasa ujue thamani ni nini kwa ujumla.

Thamani  ni vitu ambavyo unavipa kipaumbele  katika maisha na kazi yako.

Kujua thamani yako husaidia kutambua ni vitu gani katika maisha uvipe kipaumbele zaidi, kuitambua thamani yako ni kipimo tosha kitachokusaidia kuendesha maisha yako kwa namna uipendayo.

Endapo tabia  na mambo unayofanya yana ufanano na thamani yako, daima maisha huwa mazuri. ila endapo hakuna ufanano maisha huwa si sawa na huo ndio mwanzo au chanzo cha kupoteza furaha katika maisha unayoyaishi au mambo unayoyafanya katika maisha.

Thamani yako ipo, yawezekana ukawa unaitambua au huitambui. Maisha huwa rahisi endapo mtu hutambua thamani yake, kutambua thamani  husaidia kupanga mipango na kufanya maamuzi yanatayoheshimu thamani yako.

Hivyo,Tafakari ujue vitu gani katika maisha unatakiwa kuvipa kipaumbele hii itakusaidia kutambua uelekeo wa maisha yako na kufanya maamuzi sahihi.

Waziri Nchemba awanyooshea Kidole wanaomuita Rais ‘Dikteta’
Maveterani wa Jeshi Marekani washinikiza Bunge kupitisha ‘Bangi’ kama dawa