Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini Australia imethibitisha ongezeko la joto kwa kiwango cha juu ndani ya muda wa siku kumi mfululizo kilichofikia kipimo cha nyuzi joto 40.

Joto hilo lililopitiliza limekuwa likikitesa raia na viumbe hai nchini humo kwa kusababisha vifo vya mifugo, milipuko ya moto katika misitu na ongezeko la wagonjwa katika hospitili za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa wamesema vipimo vinaonyesha joto litapanda hadi kufikia nyuzi joto 42 katika baadhi ya maeneo nchini Australia.

Aidha, hali hiyo sio mara ya kwanza kwa joto kuongezeka kwa kiwango cha juu nchini Austaralia, kwani mnamo mwaka 2013 mwezi januari vipimo vilionyesha joto la nchi hiyo kuwa ni nyuzi joto 40.

Hadi kufika sasa hakuna kifo kilichoripotiwa lakini takribani watu 14 wamepelekwa hospitali kwa kuathirika na joto lililopanda siku ya jumatano na mamlaka imetoa wito kwa wananchi kupunguza kazi nzito na kulala wakiwa wameacha milango wazi.

 

 

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 19, 2019
Nikki Mbishi ampa tano Nikki wa Pili, ‘hapo ulikuwa sawa’