Jeshi la polisi nchini Tanzania limewaasa Wananchi pamoja na Viongozi katika maeneo mbalimbali kutoa taarifa juu ya vijana wanaorejea makwao kutoka mikoani ama maeneo mengine ya nchi wanaowashuku kuhusika na uhalifu.
Msemaji wa jeshi la polisi nchini, David Misime ameyasema hayo na kudai kuwa kwasasa taarifa za kuaminika zinaonesha, vikundi vya uhalifu maarufu kama ‘Panya Road’ wamekimbilia mikoa jirani baada ya jeshi la polisi kuanza utekelezwaji wa operations dhidi yao.
Mapema mwezi, Septemba, 2022 Polisi lilitangaza kuwaua kwa risasi watu sita na kuwakamata watuhumiwa 135 kwa mahojiano wakituhumiwa kuhusika na matukio mbalimbali ya uhalifu, jijini Dar es Salaam.
Aidha, Septemba 15, 2022 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alitangaza oparesheni maalum na Askari Polisi 300 waliwekwa kushughulikia suala hilo, ambapo jamii iliombwa kushirikiana na vyombo vya Dola ili kukabiliana na matukio ya uhalifu.