Katibu Mkuu wa Shirika la Nchi Zinazouza Petroli (OPEC) Mohammed Barkindo ameonya maofisa wa Umoja wa Ulaya kuhusu vikwazo kwa Urusi ambavyo amedai vinaweza kuibua mshtuko mbaya zaidi kuwahi kutokea katika historia ya usambazaji wa mafuta duniani.
Barkindo amedai kuwa mapipa milioni saba ya mafuta ya Urusi yanaondoka kila siku katika soko la dunia na kwamba hakuna mbadala wa kiwango hicho cha mafuta kinachopotea kutokana na vikwazo kwa Urusi.
Afisa huyo wa OPEC amesema shirika hilo haliwezi kulaumiwa kwa kile kinachoendelea sasa na kushauri Umoja wa Ulaya kuangalia upya na kwa uhalisia swala la nishati.
Hata hivyo Umoja wa Ulaya Umeungana na Marekani na Uingereza katika kuweka vikwazo vya bidhaa za nishati za Urusi.
Tofauti na Marekani na Uingereza, Umoja huo hutegemea zaidi nishati kutoka Urusi na wataalamu wameonya kwamba kujaribu kukata usambazaji wa nishati hiyo kunaweza kuwa na matokeo mabaya.