Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amesema jumla ya wanafunzi 73,101 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu kati ya wanafunzi 121,251 ambapo wengine wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu na vyuo vya ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).
ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA KIDATO CHA TANO.
Kati ya wanafunzi hao wa kidato cha tano waliochaguliwa, wasichana ni 35,005 sawa na asilimia 47.9 na wavulana 38,096 sawa na asilimia 52.1.
Na wanafunzi 1,572 wamechaguliwa kujiunga na shule za wanafunzi wenye ufaulu mzuri zaidi (vipaji maalumu), ikiwemo wanafunzi wanne wavulana wenye mahitaji maalumu.
Huku wanafunzi 183 ni wa mahitaji maalumu wakiwemo wasichana 82 na wavulana 101.
Aidha Jafo amesema kuwa wanafunzi wote wa bweni wanatakiwa kuripoti shuleni Julai 18, mwaka huu na masomo kuanza rasmi Julai 20, huku akiwatahadharisha watakaoshindwa kuripoti ndani ya wiki mbili tangu shule kufunguliwa nafasi zao zitachukuliwa na wengine.
Bofya linki hapa chini kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano 2020.
ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA ELIMU YA KIDATO CHA TANO.