Mwanariadha maarufu wa Afrika Kusini, Ocar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela kwa kosa la kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao (valentine’s day) Februari 14 mwaka 2013.

Hukumu hiyo iliyotolewa na Jaji Thokozile Masipa imekuja baada ya hukumu ya awali ya kosa la kuua bila kukusudiwa kubadilishwa kuwa kosa la mauaji Disemba mwaka jana baada ya upande wa mashtaka kukata rufaa.

Mwanariadha huyo mlemavu alipelekwa haraka jela kuanza kifungo chake lakini Jaji alieleza kuwa pande zote mbili bado zina nafasi ya kukata rufaa. Hata hivyo, mwanasheria wa Oscar alieleza kuwa hawatakata rufaa.

Oscar Pistorius mwenye umri wa miaka 29 alimpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp mara nne kupitia mlango wa chooni uliokuwa umefungwa.

Ingawa amekuwa akijitetea kuwa alimfyatulia risasi akidhani ni mvamizi aliyewaingilia, majirani walieleza kuwawalisikia ugomvi kati yao muda mfupi kabla ya tukio hilo na inaaminika kuwa alifanya hivyo kutokana na wivu wa mapenzi.

Ripoti: Mahakama ya Ufisadi kuanza na Lowassa
Kampuni Ya Mabasi City Boy Yafungiwa