Kiungo wa kati wa Chelsea Oscar amekanusha habari kwamba alihusika kwenye mfarakano na mchezaji mwenzake Diego Costa wakati wa mazoezi.

Gazeti la Telegraph liliripoti kwamba ilibidi wachezaji hao wawili kutenganishwa baada yao kushikana mashati Costa alipomchezea visivyo Oscar.

Lakini Oscar, mwenye umri wa miaka 24, ameandika kwenye Twitter kwamba hawezi akapigana na mchezaji mwenzake, na kumweleza mshambuliaji huyo wa Uhispania, mwenye umri wamiaka 27, kama “mmoja wa marafiki wangu wakubwa”.

Chelsea watakutana na klabu ya ligi ya daraja la tatu Scunthorpe katika raundi ya tatu ya Kombe la FA Jumapili.

Platini Akubali Kuwaachia Wengine Nafasi Ya Urais FIFA
Diamond atajwa tena tuzo kubwa Afrika