Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Baran Sillo amesema taasisi ya OSHA ni mdau mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwani wanalinda nguvu kazi ya Taifa kwa kuhakikisha maeneo ya kazi yanakuwa salama dhidi ya viararishi vya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.

Sillo ameyasema hayo wakati Kamati ya Kudumu ya Bungeya Bajeti ikihitimisha ziara ya kutembelea viwanda Mkoani Arusha na Kilimanjaro, kwa lengo la kujionea utekelezaji wa sheria na miongozo mbalimbali ya usalama na afya mahali pa kazi ikiambatana naNaibu wa Waziri – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Katambi, Katibu Mkuu, watumishiwa Ofisi hiyo naWakaguzi wa OSHA.

Amesema, “OSHA ni wadau wakubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwa sababu wanalinda nguvu kazi ya taifa ambayo ndio inazalisha, jukumu letu kubwa ni kuishauri Serikali nasi ili OSHA iendelee kuyafikia maeneo ya kazi mengi zaidi na nguvu kazi iwe salama na yenye kuzalisha na kukuza uchumi wa taifa letu.”

Kwa upande wake Katambi amesema “nguvu kazi ya taifa letu tusipo ilinda athari zake hata uchumi wetu utashuka kwasababu tutakosa wataalam na nguvu kazi itakuwa tegemezi kwa taifa na ndio maana taasisi ya OSHA inafanya kazi usiku na mchana, ili kuhakikishamaeneo ya kazi yote yanakuwa salama dhidi ya vihatarishi vya ajali na magonjwa.

Naye Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema wamekuwa ikipokea shuhuda mbalimbali kutoka kwa wamiliki wa maeneo ya kazi wakikiri kuwa kaguzi za usalama na afya pamoja na ushauri wa kitaalamu unaotolewa na OSHA vimesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza ushindani wa bidhaa wanazozalisha katika masoko ya kimataifa.

Awali Mkurugenzi wa Kampuni ya Kilimanjaro Plantation Limited, Calton Rabenold amesema, “OSHA imetusaidia kuboresha mifumo ya usalama na afya mahali pa kazi kupitia kaguzi, mafunzo pamoja na ushauri wanaotoa baada ya kubaini mapungufu na changamoto mbalimbali za kiusalama.” 

Akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Kamati hiyo ya Bajeti kwa kufanya ziara ya kutembelea viwanda hivyo pamoja na kushiriki semina elekezi ya mafunzo ya usalama na afya iliyofanyika tarehe 10/09/2023 Mkoani Arusha.

Miguel Gamondi: Sina Presha na Al Merrikh
Aubin Kramo kurudi nyumbani Ivory Coast