Klabu ya Manchester City inapewa nafasi kubwa ya kukamilisha usajili wa beki wa kati kutoka nchini Argentina na klabu ya Valencia ya Hispania Nicolás Hernán Gonzalo Otamendi.

Man City, wanapewa anfasi kubwa ya kufanya hivyo huku kiasi cha paund million 28.5 kikitajwa kutumika katika usajili wa beki huyo ambaye pia alitajwa kuwa katika mipango ya meneja wa Man Utd Louis Van Gaal.

Imeelezwa kwamba tayari amzungumzo yameshafanyika baina ya pande zote mbili na muafaka wa makubaliano umeshafikiwa, hivyo kinachosubiriwa kwa sasa ni kukamilishwa kwa sehemu ya usajili wa Otamendi.

Hata hivyo mshambuliaji Alvaro Negredo ametajwa kutumika katika sehemu ya usajili wa Otamendi, baada ya kusajiliwa kwa mkopo na klabu ya Valencia msimu uliopita na sasa amesajiliwa moja kwa moja huko Estadio Mestella.

Usajili wa Negredo kusalia Valencia umebainishwa kuwa ni kiasi cha paund million 24, ambacho hakitalipwa huko Etihad Stadium, zaidi ya Man City kutakiwa kuongeza Paund million 4.5, ili kuhitimisha mpango wa usajili wa Otamendi.

Man City wamedhamiria kuimarisha safu yao ya ulinzi kwa kumsajili Otamendi  mwenye umri wa miaka 27 ambapo atakwenda kusaidiana na Vincent Kompany, Eliaquim Mangala, Martin Demichelis pamoja na Jason Denayer.

Yanga Kuiwahi Azam FC Dar es salaam
Hamis Azigonganisha Ruvu Shooting Na Toto