Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Nasreddine Mohammed Nabi ameanza kumfuatilia Mshambuliaji wa AS Real Bamako ya Mali, Ousmane Kamissoko.

Kamissoko mwenye miaka 24, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia AS Real Bamako Julai Mosi 2022, ambao unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa kutoka Young Africans zinaeleza kuwa, tayari Nabi ameshaonesha kuvutiwa na ubora wa Kamissoko, hivyo amewataka viongozi wa Young Africans, kuanza mazungumzo mara moja na nyota huyo, kama watafanikiwa basi ataachana na Tuisila Kisinda.

“Tunamshukuru sana kocha wetu kwa kuendelea kuwa na jicho la kipekee la kufanya maboresho katika kikosi chetu, pamoja na kuwa bado tuna michezo sita ya kukamilisha msimu huu wa Ligi Kuu, ameuomba uongozi kumfuatilia Mshambuliaji AS Real Bamako, Kamissoko ili kama watafanikiwa kumshawishi aweze kuja akiwa ni mbadala wa Kisinda,” kimeeleza chanzo cha taarifa kutoka Young Africans

Mshambuliaji huyo amekuwa na kiwango bora msimu huu ambapo katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi dhidi ya TP Mazembe, Machi 19 mwaka huu alifunga mabao mawili.

Namna ya kujisajili Meridianbet Kasino ya Mtandaoni na ushinde
Kiungo Rivers Unites atuma salamu nzito Simba SC