Shirika la Kimataifa la Oxfam limetangaza kufunga Ofisi zake katika nchi 18 kutokana na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na mlipuko wa virus vya Corona.
Shirika hilo limesema kuwa wafanyakazi takribani 1,450 na taasisi 700 kati ya 1,900 ambazo wamekuwa wakishirikiaana nazo wataathirika na kufungwa kwake.
Ofisi za Shirika hilo zilizofungwa ni Tanzania, Thailand, Afghanistan, Sri Lanka, Pakistani, Tajikistan, Haiti, Dominican, Cuba, Paraguay, Misri, Sudan, Burundi, Rwanda, Sierra Leone, Benin, Liberia na Mauritania zitafungwa.
Oxfam ambayo imejikita katika kutoa misaada ya kimaendeleo imefanya kazi hapa nchini tangu miaka ya 1960 katika miradi mbalimbali ikiwemo ya Utawala na uwezeshaji wa Wanawake.