Kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Ozil amesema daima ataipenda na kuithamini klabu ya Arsenal, licha ya kuodnoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na Fenerbahceya Uturuki.
Ozil ametoa kauli hiyo kupitia barua ya wazi aliyoianika kwenye mitanbdao ya kijamii, baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu kuitumikia Fenerbahce, ambayo imemsajili kwa uhamisho huru, kufautia makubaliano yaliyofikiwa kati ya mchezaji huyo na viongozi wa Arsenal.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, amesema akiwa Arsenal alicheza kwa heshima na kuipenda klabu hiyo na mwishowe alifanikiwa kutwaa taji la FA mara tatu, huku akifunga mabao 44 katika michezo 254 kwenye michuano yote aliocheza.
“Ni vigumu kwangu kuweka kwa maneno upendo ninaohisi kwa klabu na mashabiki,” amesema Ozil kupitia barua ya wazi.
“Ninawezaje kuelezea miaka minane ya shukrani kwa barua moja?…. Nitakuwa Gunner kwa maisha yote – bila shaka juu ya hilo.”
Ozil alijiunga na Washika Bunduki akitokea Real Madrid kwa pauni milioni 42.4 mnamo 2013 ikiwa ni ada ya uhamisho wa rekodi ya klabu na akaanza vizuri waliposhinda Kombe la FA msimu wake wa kwanza akimaliza kusubiri kombe kwa miaka tisa.
Alicheza michezo 32 msimu wa 2014-15, licha ya kukosa miezi mitatu na jeraha la goti, na akashinda Kombe la FA kwa mwaka wa pili mfululizo.
Katika msimu uliofuata alitoa pasi 19 zilizo zaa mabao katika msimu, moja tu nyuma ya rekodi za Ligi ya England (Premier League) ambayo sasa inashikiliwa na Thierry Henry na Kevin de Bruyne.
Alikuwa pia mchezaji wa kwanza kutengeneza goli katika michezo sita mfululizo na aliteuliwa kuwa mchezaji Bora wa msimu kwa Arsenal.
Alikuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya klabu mnamo Januari 2018, akisaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu akilipwa takriban Pauni 350,000 kwa juma.
Ozil, mshindi wa Kombe la Dunia la 2014 na Ujerumani ambaye alistaafu soka kimataifa, alianza kupigishwa benchi chini ya meneja wa zamani wa Arsenal Unai Emery, kabla ya kurudi uwanjani chini ya Kocha wa Muda Freddie Ljungberg.
Baada ya uteuzi wa Mikel Arteta mnamo Disemba 2019, Ozil alianza michezo yote 10 ya PL, Arsenal mara moja kabla ya janga la coronavirus mnamo Machi na baada ya hapo hakuichezea klabu tena. Mnamo Oktoba 2020 aliachwa kwenye vikosi vya wachezaji 25 vya Arsenal kwa Europa League na Premier League.