Tuzo za BET zimegeuka kuwa mwimba wa ubaguzi kwa wasanii wa Afrika na Uingereza wanaowania vipengele vya vya Best International Act: Africa na ‘Best International Act: UK.

Katika kuonesha hisia zao bila kuficha ugonjwa, baadhi ya wasanii wa Afrika wameamua kuwatolea uvivu waandaaji wa tuzo hizo.

Wizkid Ayo na Fuse ODG ni kati ya wasanii wa Afrika ambao wametumia akaunti zao za twitter kuwafikishia BET uamuzi wao wa kuzisusia tuzo hizo zilizotolewa wikendi iliyopita katika ukumbi wa Microsoft Theater, Los Angeles, California.
Kupitia akaunti yake ya Twitter, Wizkid ameeleza BET kuwa anajua wamemkasirikia kwa kutohudhuria tuzo hizo kama walivyotarajia lakini msimamo wake unatokana na tabia ya kupewa tuzo hizo nyumba ya jukwaa.
“Lakini sitakuwa nahudhuria show zenu za utangulizi na sherehe za waliotajwa kuwania tuzo hizo kama ninapewa tuzo saa nne asubuhi kabla ya show yenyewe,” alieza Wizkid kupitia twitter.
Wizkid alieleza kuwa alikuwa palepale Los Angeles lakini aliamua tu kuangalia show ya tuzo hizo kwa sababu anawapenda. Tweets za Wizkid ziliungwa mkono na kaka wa P’Square, Jude Okooye ambaye huenda akachukuliwa kama amewakilisha mtazamo wa P’Square.

TWEET P
Jana mkali wa Azonto, Fuse ODG aliwachana kwa kuwataja waandaaji wa BET na kuweka wazi uamuzi wake wa kuzisusia tuzo hizo zinazobagua washindi wa kipengele cha ‘Best International Act: Africa’.
Washindi wa vipengele vya ‘Best International Act: Africa na Best International Act: UK hutangazwa mapema na kukabidhiwa tuzo zao bila kulikanyaga jukwaa kubwa la tuzo hizo zilizolenga katika kuwatunuku na kutambua zaidi mchango wa watu weusi katika kiwanda cha muziki.

Video Mpya: Ali Kiba – Chekecha Cheketua
Ronaldinho Arejea Ulaya, Kucheza na Pacha Wake Antalyaspor