Pacha wenye jinsia ya kike waliozaliwa wakiwa wameungana kichwani na kisha mwaka jana kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa na timu ya madaktari bingwa takribani 100 katika Hospitali ya Great Ormond Street ya jijini London, wameruhusiwa kwenda nyumbani kwao nchini Pakistan.

Watoto hao Safa na Marwa kabla ya kuruhusiwa walifanyiwa upasuaji mkubwa mara tatu na kutumia takribani saa 50 katika chumba cha upasuaji.

Mama mzazi wa watoto hao, Zainab amesema anafuraha baada kuwarejesha watoto wake nyumbani kwa ajili ya kuungana na wenzao.

“Mabinti wanaendelea vizuri sana, Marwa amekuwa na maendeleo mazuri na kwamba anahitaji msaada mdogo,” amesema mama huyo.

“Tutaendelea kumwangalia kwa karibu zaidi Safa na kumpa matunzo mazuri. Kwa uwezo wa Mungu, wote wawili wataanza kutembea.”

NEC yaifuta adhabu ya Mbatia
Mtibwa Sugar wanatufundisha jambo