Mabingwa wa soka duniani, klabu ya Real Madrid watalazimika kuuza mchezaji anaecheza nafasi ya ushambuliaji, ili kufanikisha usajili wa mpachika mabao wa Juventus Paulo Dybala itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Dybala amekua katika mipango ya usajili wa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, baada ua kuonyesha uwezo mkubwa wa kupachika mabao kwenye ligi ya nchini Italia.

Zidane tayari ameshamuomba rais wa Real Madrid Florentino Perez kufanya kila analoweza ili amsajili mshambuliaji huyo raia wa nchini Argentina.

Mchambulizi wa soka Paco Gonzalez, amezungumza na El Partidazo, na kusema kuwa: “Itatulazimu kusubiri ili kuona uwezekano wa usajili wa Dybala kama utakamilishwa. Lakini ninavyojua ni kwamba, kama kweli Dybala anatakiwa Bernabeu ni lazima mshambuliaji mmoja kati ya James (Rodriguez) na (Karim) Benzema auzwe.

“Itakua vigumu kwa mchezaji kama Dybala kusajiliwa Real Madrid halafu akaenda kukaa benchi, ni lazima atatafutiwa namna ya kucheza kama ilivyo sasa akiwa na Juventus FC. Nafahamu atawagharimu zaidi ya Euro milioni 100, na kwa kiwango hicho cha pesa huwezi kufanya mzaha wa kutomchezesha.”

Rais Magufuli aitaka Mahakama kufuatilia deni la Trilioni 7.3
Makamba azindua bodi ya taifa ya hifadhi mazingira