Padri Jacques Hamel wa kanisa katoliki ameuawa leo akiwa kanisani baada ya watu wawili wenye silaha kuvamia katika nyumba hiyo ya ibada, kaskazini mwa Ufaransa.

Watu hao wenye silaha ambao walijitambulisha kuwa ni washirika wa kundi la kigaidi linalojiita Islamic State (IS) walitekeleza tukio hilo wakati wa ibada ya asubuhi ambapo mbali na mauaji hayo waliwashikilia mateka kwa muda watu wengine wanne.

Maafisa wa Jeshi la Polisi waliwaeleza wana habari kuwa polisi walifanikiwa kuwaua watu hao muda mfupi baadae na kuwakimbiza majeruhi hospitalini.

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande alitembelea eneo hilo la tukio ambapo alieleza kuwa washambuliaji hao walifanya mauaji ya kiuwoga huku akisisitiza kuwa Ufaransa itaendelea kupambana na IS kwa njia zote.

Naye Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amelaani mauaji hayo aliyoyaita kuwa ya ‘maumivu’.

Mmoja kati ya washambuliaji hao aliyetambulika kwa jina la Adele K mwenye umri wa miaka 18, alidaiwa kuwahi kukamatwa na kuwekwa rumande na baadae kuachiwa akiwekwa chini ya amri ya udhibiti.

Makanisa 47,000 yawekwa chini ya tahadhari baada ya IS kumuua kikatili Padri kanisani
Serengeti Boys Kuweka Kambi Madagascar