Mabingwa wa soka Chile, Colo Colo walishindwa kukabidhiwa kombe lao baada ya vurugu kubwa kuzuka uwanjani na kusababisha mechi dhidi ya Santiago Wanderers kuvunjwa.

Mechi hiyo imevunjika kutokana na vurugu kubwa, huku ikionekana mashabiki wa Santiago hawakuwa tayari kuona wale wa Colo Colo wakikabidhiwa kombe.

Mashabiki wa Santiago ndiyo waliamua kushuka uwanjani na kuonyesha wazi wanataka kuzuia mchezo huo.


Wale wa Colo Colo ambao wanaamini wao ni wababe zaidi, nao walishuka uwanjani na kusababisha mwamuzi kuzuia mchezo huo wa Ligi Kuu Chile maarufu kama Primera Division, kuvunjwa.


Mashabiki hao waliendelea kutwangana kwa fimbo, mawe, viti na silaha nyingine.

Wakenya Wamchenjia Kenyatta, Wamkaribisha Upya Kenya
Arsene Wenger Aanza Kukiri Arsenal Yake Ina Pancha