Serikali ya Palestina imekataa wito wa Marekani kutaka sehemu ya Ukuta wa Magharibi katika Mji Mkongwe wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, huku ikiendelea kufanya mazishi ya wananchi wake waliouawa kwenye maandamano ya kupinga hatua hiyo.

Kiongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya Palestina, Nabil Abu Rudeineh, amesema kuwa kamwe Wapalestina hawatakubali mabadiliko yoyote kwenye mpaka wa 1967 wa Jerusalem Mashariki.

“Msimamo huu wa Marekani unathibitisha kwa mara nyingine kwamba utawala wa sasa wa nchi hiyo haupo kabisa kwenye suala la majadiliano ya kupata amani na badala yake unataka kuuimarisha mgogoro huu kwa kutaka kuugawa mji wa Jerusalem kwa mabavu,” amesema Rudeineh

Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa ziara ya makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence katika nchi za Misri, Israel na Ujerumani, kiongozi wa ngazi ya juu wa nchi hiyo alisema kuwa nchi hiyo haioni haja ya kuugawa mji wa Jerusalem kwani ni mali ya Israel.

Magazeti ya Tanzania leo Desemba 17, 2017
Mnangangwa: Huu si wakati wa kutambiana na kusifiana