Katibu Mkuu Pamba FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ‘Championship’, Johnson James, amefunguka kwamba, wameweka mikakati mizito kwa ajili ya mechi yao ya mtoano dhidi ya Mashujaa inayotarajiwa kupigwa Mei 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

James amesema: “Kikosi kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi yetu ya mtoano dhidi ya Mashujaa ambayo tunaamini mchezo utakuwa mgumu sana kutokana malengo ya timu zote mbili kupata ushindi.

“Huu ni msimu wetu wa tatu mfululizo ambao tunacheza mechi za mtoano, hatukufanikiwa misimu miwili ya nyuma, lakini msimu huu tumedhamiria kufikia malengo yetu.

“Kocha Mkuu Yusuf Chipo pamoja na benchi lake la ufundi wameweka mikakati mizuri kwa ajili ya mechi hiyo ambayo hatuwezi kuruhusu kudondosha alama yoyote.”

Ndio hivyo tena, wanasepa FC Bayern Munich
Jamii yatakiwa kuepuka uharibifu wa Mazingira