Msimamizi wa Tafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine – SUA, Saidi Mshana amesema wanyama aina ya panya buku hupatiwa mafunzo mbalimbali katika chuo cha Sokoine ambao wanatambua vimelea vya kifua kikuu na wengine wakipatiwa mafunzo ya utambuzi wa mabomu ya ardhini.

Mshana ameyasema hayo wakati akizungumza na Dar24 Media na kuelezea mafanikio ya tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa na panya hao na kwamba tafiti za kuwafundisha panya hao zimesaidia pia katika utambuzi wa magonjwa hususa ugonjwa wa kifua kikuuu ambapo anaweza kutumia dakika 10 hadi 15 kutambua vimelea hivyo.

Amesema, “Tafiti za awali zilianza kuwafundisha panya buku katika utambuzi wa mabomu ya kuzika ardhnini mradi ambao ulipata mafanikio makubwa na mpaka sasa panya hao wanafanya kazi kwenye nchi mbalimbali ili kuweza kusaidia kuondoa tatizo la mabomu ya ardhini.”

Aidha ameongeza kuwa, “tumekuwa na mchango mkubwa wa kuweza kuibua au kugundua wagonjwa wa kifua kikuu katika hatua za awali kabisa na kuweza kupata matibabu mapema zaidi.”

Amesema, Chuo hicho kinaendelea na tafiti zingine za kutumia Panya buku ambapo wanafundisha kutafuta watu waliokwama kwenye majengo kutokana na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi aua ajali za majengo kubomkoa au kufukiwa na kifusi katika maeneo ya migodi.

Mbali na hivyo kunatafiti zingine bado zipo na zinaendelea na kuna panya wengine aina hii ya panya buku sasa hivi tunawafundisha katika utafutaji wa nyara za wanyama pori kwahiyo kuna utafiti unaendelea kunusu nyara za wanyamapori na hawa tunalenga kusaidia serikali na taasisi zingine wakiwepo TAWA ambao wanamamlaka ya kusimamia wanyama pori.

Majaliwa atoa siku 7 kwa TARULA, DAWASA kukamilisha Barabara
Twaha Kiduku: Ninaogopa Sindano kuliko ngumi ya mpinzani