Mkuu wa kanisa katoliki Duniani, Papa Francis ameomba msamaha kwa naiaba ya wakristu wote wanaosapoti na kushiriki biashara haramu ya uchangudoa.
Blessing Okoedion, ambaye alilazimishwa kufanya biashara ya uchangudoa na baadae kutoroka amelaumu kwa kusema kivipi kanisa linaruhusu wanaume wa kikatoliki kununua wanawake wa Kinigeria na kushiriki nao tendo la ndoa kinyume na sheria.
Papa mejibu tuhuma hizo amesema, wanaume wote wanaosapoti na kushiriki biashara ya uchangudoa ni wauaji ambao akili zao zimeharibikiwa.
Papa Francis amesema hayo pindi akifanya mazungumzo na vijana 300 ambao aliwaalika Vatican Rome, wiki hii ili kuwasaidia viongozi wa kanisa kujifunza vitu mbalimbali ambavyo vijana wa siku hizi wanafikiria juu ya kanisa katoliki.
Katika mazungumzo hayo Papa amesema vijana wadogo wanapaswa kupiga vita biashara hizo za kuuza miili.
‘’Amesema hii ni moja ya vita ambayo ningewaomba nyie vijana wadogo kupambana navyo, kwa ajili ya kupigania utu wa mwanamke’’
Kufuatia mijadala hiyo Papa alitumia nafasi hiyo kuomba msamaha juu ya wakatoliki wote wanaojihusisha na dhambi hiyo ya biashara haramu ya kuuza na kunua mwili.
Aidha papa Francis amewasisitiza vijana wote wa dini zote kupiga vita biashara haramu hasa zile ambazo zinavunja utu wa mtu