Aliyekuwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki na kujiuzulu mwaka 2013, Papa Benedict amekiri makosa yalitokea katika kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia alipokuwa Askofu Mkuu wa Munich, na kuomba msamaha. Hata hivyo Mawakili wake wanadai hakuwa wa kulaumiwa moja kwa moja.

Taarifa ya Vatican ilitoa barua ambayo imeandikwa na Papa siku ya Jumanne 08 Februari, 2022 ya kukiri makosa yake na kuonesha mapungufu yake alipokuwa uongozini kwa kanisa katoliki kwa mwaka 1945 hadi 2019.

“Ninahusika kwa namna kubwa katika kanisa katoliki. Kwa ukubwa zaidi ni maumivu yangu kwa unyanyasaji wa kijinsia na matukio mabaya yaliyotokea wakati wa uongozi wangu wakati katika maeneo tofauti ya kanisa katoliki,” aliandika Papa Benedicto.

“Nimeelewa kwamba sisi wenyewe tunavutwa kwenye matukio haya baada ya kushindwa kukubali makosa yetu pale tunapokataa au kushindwa kuchukua hatua muhimu na kufanyia kazi yote mabaya kwa kuamini hayawezekani na wakati huo yakiendelea kutukia, kwa mara nyingine tena naendelea kuomba radhi kwa wote waliofikwa na haya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, na ninapokea aibu kubwa niliyoisababisha nikiwa na huzuni kubwa ninaomba kusamehew,” aliongeza Papa Benedicto.

Hatua hiyo inakuja kufuatia Ripoti ya unyanyasaji wa kijinsia kati ya Mwaka 1945 – 2019 iliyotolewa Mwezi Januari 2022 na Wachunguzi wa Ujerumani

Katika Uchunguzi huo, Benedict (94) aliyekuwa Askofu Mkuu wa Munich kati ya 1977 na 1982 anatuhumiwa kushindwa kuchukua hatua katika Visa vinne vya unyanyasaji wa Watoto kingono uliodaiwa kufanywa na Mapadri

Benecto ambae kwa sasa yupo katika hali ya maradhi na udhaifu wa mwili ameomba kundi la wanasheria wake kuendelea kumsaidia kusimamia swala hilo.

Katika barua yake pia Benedicto alisema kuwa pamoja na yote hayo ambayo yametajwa kuwa ni makosa yake, lakini anaamini kuwa Mungu pekee ndie anayeweza kutoa hukumu, “siku chache zijazo nitakua mbele ya Mungu nikikutana na hukumu yangu ya maisha yangu,” aliongeza Benedicto.

Uchunguzi wa Ujerumani kuhusiana na Kanisa Katoliki umebaini, Papa wa zamani Benedict XVI alishindwa kuchukua hatua dhidi ya visa vya watoto wanne walionyanyaswa alipokuwa askofu mkuu wa Munich.

Unyanyasadi uliendelea chini ya uongozi wake, imedai ripoti hiyo, na kuongeza kuwa washukiwa wa unyanyaji huo waliendelea kuwa na nyadhifa za kanisa.

Papa huyo wa zamani , ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 94, alikuwa Kiongozi wa Kanisa wa 600, mwaka 2013. Tangu wakati huo amekuwa akiishi maisha ya ukimya katika mji wa Vatcan.

Ripoti mpya, iliyoitishwa na Kanisa Katoliki, alidai aliambiwa kuhusu taarifa za unyanyasaji wa watoto wakati alipokuwa akikaimu kama Askofu mkuu, lakini hakuchukua hatua.

“Visa viwili kati ya visa hivi vya unyamyasaji, vilitekelezwa wakati wa uongozi wake,” wakili Martin Pusch alisema alipokuwa akitangaza ripoti.

“Katika matukio yote mawili, washukiwa waliendelea kufanya kazi ya kuhuduu kama wachungaji.” Alisema.

Papa Benedict alijiuzulu baada ya karibu miaka minane madarakani na kuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki kuachia madaraka kwa hiari baada ya kipindi cha miaka 600.

ATCL yaagizwa kufanya mapitio ya nauli zinazotozwa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 9, 2022