Kiongozi wa Kanisa katoliki Duniani, Papa Francis anatarajia kuzuru nchi ya Iraq Machi 5 hadi 8, mwakani ikiwa ni ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kuanza kwa janga la COVID-19.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Vatican Matteo Bruni imeeleza kwamba Papa Francis atafanya ziara ya kitume katika Jamhuri ya Iraq kuanzia Machi 5 hadi 8, 2021, ambapo atazuru mji wa Baghdad, eneo la Ur, jiji la Erbil, pamoja na Mosul na Qaraqosh katika Bonde la Ninawi.

” Ziara hii ya kipekee ya Papa inaashiria ujumbe wa amani kwa Iraq na kwa ukanda mzima,” imeeleza taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Iraq.

Kwa muda mrefu Papa Francis ambaye ana umri wa miaka 83 amekuwa akuzungumzia nia yake ya kutembelea nchi hiyo ya Mashariki ya Kati ambako mapigano yamesababisha idadi ya watu kupungua kwa kasi katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.

Kabla ya janga la Corona, Papa Francis alikuwa ameeleza wazi nia yake ya kutembelea nchi hiyo na wakati akipokea wawakilishi wa huduma za misaada kwa Makanisa ya Mashariki mwezi Juni 2019, papa Francis alielezea ‘nia’ yake ya kuzuru nchi ya Iraq mwaka 2020.

Mwezi Januari 2020 Papa Francis alimpokea huko Vatican rais wa Iraq, Barham Salih.

Azam FC kujipanga upya VPL, wapata alama mbili kanda ya ziwa
Lwanga kamiligado Simba SC