Papa Francis ameagiza kupigwa marufuku kwa uuzaji wa sigara ndani ya Vatican kuanzia mwaka ujao ili kuweza kunusuru afya za raia.

Hayo yamesemwa na Msemaji wa Vatican, Greg Burke ambapo amesema kuwa mji huo mtakatifu hauwezi kukubaliana na kitendo ambacho kinahatarisha maisha ya binaadamu kwa ujumla.

Aidha, takriban wafanyikazi 5000 wa Vatican na wale waliostaafu wanakibali cha kununua sigara zilizopunguzwa bei, ambapo mauzo hayo yanasemekana kuiingizia mapato ya mamilioni Vatican kwa mwaka.

Msemaji wa Vatican, Burke ameongeza kuwa hakuna faida ambayo ni halali iwapo sigara zinaathiri afya za wanaadamu, huku akisema takwimu za shirika la afya duniani WHO ambazo zinalaumu uvutaji sigara kuwa zinasababisha vifo vya takriban watu miioni 7 duniani kila mwaka.

”Nadhani watu wengi wanapenda sigara kwa sababu ya ufadhili wanaoupata, kitu hiki ni lazima kifutwe licha ya kuleta mapato Vatican, muhimu ni kufanya kile kilicho sawa,”amesema Burke.

 

 

Malinzi, Mwesigwa wakwama mahakamani
Dkt. Willbroad Slaa ageuka mhudumu Canada