Papa Francis anasafiri Iraq leo Ijumaa katika ziara ya kwanza rasmi nchini humo na safari yake ya kwanza ya kimataifa tangu kuzuka kwa janga la corona ambapo takribani wanajeshi 10,000 wa Iraq watalinda ulinzi wakati wa ziara hiyo.

Safari hiyo ya siku nne inakusudiwa kuihakikishia jamii ya Kikristo inayopungua ya Iraq na kukuza mazungumzo kati ya dini.

Papa atakutana na Kiongozi wa Waislamu wa dhehebu la Kishia anayeheshimiwa sana, na kufanya sala huko Mosul na kuhudhuria misa katika uwanja wa michezo.

Amesisitiza kufanya ziara hiyo licha ya ongezeko jipya la maambukizi ya Covid-19 nchini Iraq na hofu dhidi ya usalama wake.

Papa John Paul wa pili alifuta mpango wa safari yake nchini humo mwisho wa mwaka 1999 baada ya mazungumzo kati yake na Rais wa wakati huo Saddam Hussein kuvunjika.

Ndani ya miongo miwili tangu wakati huo, moja ya jamii ya zamani ya Wakristo duniani imeshuhudia idadi yake ikipungua kutoka milioni 1.4 hadi karibu watu 250,000.

Baadhi yao wamekimbilia ughaibuni kwa kuhofia mashambulio kwa misingi ya kidini ambayo yamekumba nchi hiyo tangu Marekani ilipoivamia kijeshi mwaka 2003 na kumuondoa madarakani Saddam Hussein.

Trump kufunguliwa tena YouTube
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 5, 2021