Klabu ya Simba SC imefikia makubaliano na Klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa katika usajili wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Senegal Pape Osmane Sakho.
Simba SC imethibitika kufanywa kwa biashara hiyo mapema leo Jumatatu (Julai 24) kuptia vyanzo vya habari vya klabu hiyo ya jijini Dar es salaam.
Taarifa iliyothibitisha kuondoka kwa Kiungo huyo imeeleza: Simba SC tumefikia makubaliano na klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) ya nchini Ufaransa kumnunua mchezaji wetu.
Tunamtakia kila la kheri Sakho kwenye timu yake mpya. Kwa taarifa zaidi ingia kwenye Simba App. #NguvuMoja
Takwimu za Sakho tangu ajiunge na Simba Sc
??21/22 – Magoli 6
??22/23 – Magoli 9
Hata hivyo taarifa ambazo hazijathibitishwa na Uongozi wa Klabu ya Simba SC zinaeleza kuwa Sakho ameuzwa kwa ada ya uhamisho isiyopungua Bilioni 2.