Mlinzi wa kati kutoka nchini Ivory Coast Pascal Wawa, amesema watapambana pasina kuchoka dhidi ya FC Platnum, katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, utakaounguruma Jumatano (Desemba 23) mjini Harare, Zimbabwe.

Wawa amesema wamekwenda ugenini kupambana kama ilivyokua kwenye mchezo uliopita dhidi ya Plateau United, hivyo kila mmoja wao amekua akihamasika na ushawishi wa kuhakikisha wanamaliza dakika 90 za mchezo huo kwa faida.

“Tutahakikisha tunapambana kufanya vizuri kwenye mchezo wetu kwa kuwa malengo yetu ni kuona kwamba timu inafika mbali kimataifa.

“Ili kufika huko hatuna namna ni lazima tupambane kupata matokeo chanya ndani ya uwanja hivyo mashabiki wazidi kutuombea dua.” Amesema Wawa.

Kikosi cha wachezaji 22 cha Simba SC kimeweka kambi mjini Harare tangu Ijumaa (Desemba 18), na tayari kinaendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya FC Platnum tangu Jumamosi (Desemba 19).

KMC FC watinga Dodoma kuibali JKT Tanzania
Kata 27 hazina shule za sekondari- Rukwa