Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk.Anna Makakala, amesema wapo kwenye mchakato wa kuanzisha hati mpya za kusafiria za kielekroniki ambazo zitakuwa na vigezo vya usalama vya kimataifa.

Amesema uamuzi wa kuanzisha hati hizo umetokana na makubaliano yaliyopitishwa na wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC, lengo ikiwa ni kuimarisha ulinzi na usalama.

‘Kuna mabadiliko makubwa ya kiteknolijia katika dunia na ukiangalia katika nchi zilizoendelea, tayari wenzetu walishaanza muda mrefu’. Amesema Makakala.

Ambapo ameeleza kuwa Passport mtandao ni kadi ambayo ikiingizwa kwenye mashine taarifa zote za mtumiaji huonekana kutokana na teknolojia hiyo usalama na ulinzi utakuwa umeimarika zaidi.

Hata hivyo amesema kuwa taratibu hizo zote zinatarajiwa kumalizika na kuanza kutolewa rasmi baada ya miaka miwili na matumizi yake yataenda sambamba na passport ya sasa hadi zile zilizopo mononi mwa watu muda wake kuisha.

Ofisi za UN zavamiwa nchini Burundi
Dimitry Seluk kumtibua tena Guardiola?