Katika hali isiyokuwa ya kawaida kiongozi mmoja wa dini nchini Ghana ameonekana akiwavua wanawake nguo kanisani na kuwaogesha, tukio linalosadikika kuwa lilifanyika siku ya mkesha wa mwaka mpya, wiki iliyopita.

Katika video inayosambaa mtandaoni, pasta huyo anasikika akiwambia ‘kondoo wake wa kike’ wajitokeze haraka kwa “kuoga takatifu.”

Katika kipande cha video kilichosambaa mitandaoni, wanawake wanaonekana wakivua nguo na mbele ya ‘mchungaji huyo’ na kisha wanaingia kwenye beseni kubwa kuogeshwa upako.

Mchungaji huyo pia anasikika akisema kuwa licha ya kufahamu kwamba hatua hiyo itazua utata, hana budi ila kuheshimu maagizo ya Roho Mtakatifu.

Wakati tukio hilo likijiri kuukaribisha mwaka mpya na wakati tukifunga mwaka wa 2021 nchini Ghana, huko nchini Nigeria pia Mchungaji mwingine anayefahamika kama J.S. Yusuf, anadaiwa kuzindua nguo za ndani za kike (chupi) zenye picha yake pamoja na sidiria zenye chapa ya picha yake.

Kiongozi huyo amenukuliwa akisema amefanya hivyo ili kuwasaidia wanawake waseja wanaotamani kuolewa kuwavizia waume zao.

Kulingana na maelezo ya Mchungaji Yusuf, ambaye ni mkuu wa Kanisa la Touch for Recovery Outreach International la mjini Abuja, aliagizwa na Mungu kuzindua nguo hizo za ‘baraka’ ili kufungua milango ya ndoa kwa Mwaka Mpya.

Mchungaji huyo alinukuu mstari kwenye kitabu cha Hesabu 23:20 unaosema “Tazama nimepokea amri ya kubariki, naye amebariki, wala siwezi kubadili.”

Pia, alisema kuwa nguo hizo zinapovaliwa na wanawake, zitawasaidia kupigana na magonjwa na kupata bahati njema ya kuwavizia wanaume ambao watawaoa.

Hayo ni mambo ya imani, dunia ina mambo mengi, unachagua kuamini na kutoamini lipi? Kazi ni kwako. Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni.

Vyombo vya usalama barabarani vyatakiwa kuwa makini
Ahmed Ally akalia kiti cha Manara Simba SC