Msanii wa Nigeria, Patoranking amesema kuwa bado yuko ‘single’ na kwamba anatafuta mwanamke wa kufunga ndoa ambaye amezitaja sifa zake.

Akiongea na katika kipindi cha Route 919 cha 91.9 Live Fm nchini humo, Patoranking alisema kuwa anatafuta mwanamke mwenye tabia nzuri ambaye sifa zake ni zaidi ya mwenekano mzuri atakaokuwa nao.

Mkali huyo wa ngoma ya ‘My Woman My Everything’ alisema anataka mwanamke ambaye atakuwa na sifa za kipekee kama ametoka kwenye dunia nyingine tofauti na wengi anaowaona.

“Sipelekwi na kitu chochote tu, nahitaji kitu ambacho kitadumu zaidi. Namaanisha kama nitahudhuria maonesho ya mitindo, nitakutana na wanawake wengi ambao ni wazuri zaidi ya mke wangu kwahiyo tabia zake ndizo zitakazomtofautisha na wengine,” alisema.

Mwanzilishi wa Facebook Atangaza Kuwapa Masikini 99% ya hisa zake
Mpango wa Ukawa Kuunda Chama Kimoja Cha Siasa Huu Hapa