Aliyekuwa kocha wa Zamalek SC ya Misri Patrice Carteron amekamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Al-Taawon inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia.

Carteron amejiunga na klabu hiyo na atatambulika kama mkuu wa benchi la Ufundi, huku kazi kubwa aliyokabidhiwa ni kuhakkisha Al-Taawon inatwa mataji ya ndani nan je ya Saudi Arabia.

Kocha huyo kutoka nchini Ufaransa amewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na TP Mazembe mwaka 2015 na mataji mawili ya CAF Super Cup na Raja Casablanca (2019) na kisha Zamalek SC (2020).

Imeripotiwa kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 atapokea karibu Dola 500,000 sawa na shilingi za kitanzania Bilioni 1.2 kama mshahara wake kila mwezi.

Klabu nyingine alizowahi kuzitumikia ni Cannes (2008–2009), Dijon (2009–2012  ), TP Mazembe (2013–2016), Wadi Degla (2016–2016), Al-Nassr (2017–2017), Phoenix Rising (2017–2018), Al Ahly (2018–2018),  Raja Casablanca (2019–2019) na Zamalek SC (2019–2020).

Kati ya mwaka 2012–2013 Patrice Carteron alifanya kazi kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Mali.

The Cranes: Rais Museveni timiza ahadi yako
TCAA yaruhusu ndege za Kenya

Comments

comments