Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ Patrice Motsepe anaamini Afrika ina nafasi kubwa ya kutinga kwenye mchezo wa Fainali kuanzia Fainali zijazo za 2026 zitakazounguruma katika nchi za Mexico, Merakani na Canada.

Kwa mara ya kwanza Afrika ilivunja Rekodi yake kwa kushuhudia Timu ya Taifa ya Morocco ikifika kwa mara ya kwanza Hatua ya Nusu Fainali katika Fainali zilizomalizika Desemba 18 nchini Qatar, ikivuka Rekodi iliyowekwa na Cameroon mwaka 1990, Senegal mwaka 2022 na Ghana mwaka 2010 zilizoishia Hatua ya Robo Fainali.

Rais Motsepe ameweka wazi matarajio hayo alipozungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano maalum, baada ya kurejea kutoka nchini Qatar zilipopigwa Fainali za Kombe la Dunia 2022.

“Ni matumaini makubwa kwamba katika Fainali zijazo za Kombe la Dunia, Afrika itapiga hatua kubwa zaidi, itavuka Hatua ya Nusu Fainali za kutinga Fainali,”

“Morocco imeonesha kuwa inawezekana, imetuheshimisha waafrika ambao siku zote tuliamini hatuwezi kuvuka Robo Fainali, lakini mwaka huu Dunia imeona kuwa Afrika inaweza kusogea, Binafsi ninaamini kuanzia mwaka 2026 tutakwenda kuishangaza maradufu Dunia.”

“Kama utaangalia na kufautilia vizuri, Afrika imekua na vipaji vikubwa kwa vijana, ninaamini hawa ndio watakua Mashujaa wa kutuvusha kutoka Nusu Fainali na kutupeleka Fainali, katika Fainali zijazo tutakuwa na Timu Tisa, ninaamini kwa wingi wa timu zetu, tutaweza kuwakilishwa vizuri, tena kwa mafanikio.” amesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 60.

Katika Fainali za Kombe la Dunia 2022, Afrika iliwakilishwa na mataifa matano ambayo ni Senegal, Cameroon, Morocco, Tunisia na Ghana.

Uongozi Young Africans wamsusia Nasreddine Nabi
Bwawa la Nyerere litasaidia kuzuia mafuriko