Mshambuliaji kinda wa klabu ya Chelsea, Patrick Bamford amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Crystal Palace kwa mkopo wa muda mrefu.

Bamford, mwenye umri wa miaka 21, alionyesha umahiri wa kucheza kwa kujituma msimu uliopita baada ya kupelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Middlesbrough inayoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza nchini Uingereza.

Akiwa na klabu hiyo msimu uliopita, Bamford alifanikiwa kupachika mabao 17, hatua ambayo ilichochea kutunukiwa tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo.

Bamford, ambaye pia ni mchezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, chini ya umri wa miaka 21, aliwahi kutolewa kwa mkopo katika baadhi ya klabu nchini humo kama MK Dons pamoja Derby county.

Chelsea walifanikiwa kumnasa mchezaji huyo, baada ya kumfuatilia kwa kipindi kirefu kwenye kituo cha kulea na kuendeleza vipaji cha klabu ya Nottingham Forest.

Esteban Cambiasso Akataa Kuendelea Na Leicester City
Juventus Wafunguliwa Dirisha Kumalizana Na Julian Draxler