Mkongwe wa Liverpool, Paul Ince anaamini Bruno Fernandes hana sifa ya kuwa kiungo wa timu hiyo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29, alipewa kitambaa cha unahodha na Kocha Erik ten Hag akichukua baada ya Harry Maguire kuvuliwa.
Lakini mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 56 aliyewahi kuichezea Liverpool na timu ya taifa England mwaka 1993, hana uhakika kama Bruno anafati kuwa nahodha.
Akizumgumza kupitia talkSPORT, alisema: “Sijui namwonaje Bruno, sielewi kama ni kiongozi jinsi anavyocheza, hivi kweli ni kiongozi? Kwa sasa kiwango chake sio kikubwa kivile, ndio alifunga bao la ushindi dhidi ya Fulham.
Lakini kama kiongozi unatakiwa kuwa na mpangilio mzuri, niliwahi kuwa nahodha na nilijivunia sana, nikiona kiwango changu sio kizuri nawahimiza wenzangu wapambane, nahodha mzuri ni yule anayefahamu wachezaji wenzake vizuri, unapomwangalia Bruno kuna wakati mwingine anajifikiria yeye tu, anapokuwa hachezi vizuri utaona vitendo vyake.”
Mkongwe wa Man United, Roy Keane aliwahi kumponda Bruno kutokana na vitendo vyake katika mechi ya Ligi Kuu England ya Manchester Derby, mashetani wekundu ikipokea kichapo cha mabao 3-0.
“Kwa jinsi nilichokiona katika mechi dhidi ya Man City ningemvua unahodha asilimia 100, najua maamuzi ni makubwa sana, alibadilishana na Harry Maguire, lakini ukweli Bruno hana sifa ya kuwa nahodha, nafikiri ni mchezaji mzuri lakini unahodha? hapana.”
Wakati huo huo, Keane alimsemna Bruno baada ya kukubali kumpa Marcus Rashford Penati katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Everton mwishoni mwa juma lililopita.
Takwimu zinaonyesha Man United ilishinda mechi tano kati ya mechi sita za mwisho na kuendelea kujikita nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, na mwishoni mwa juma hili itacheza dhidi ya Newcastle.